MAMBO 10 YA KUMFANYA MPENZI WAKO AKUPENDE MILELE

Wewe kama mwanamme au mwanamke, najua unahitaji sana kulitunza penzi lako na kufanya lidumu milele kama wenyewe mnavyosema. Lakini wacha nikwambie kutunza penzi si ghalama kama watu wengi wanavyodhani, ila kuna vitu vichache ambavyo ukivifanya basi utadumu naye. Maana ingekuwa mapenzi ni ghalama basi maskini wasinge dumu kwenye mapenzi yao, lakini badala yake maskini ndiyo wanaongoza kudumu katika ndoa Na hizi ni hatua 10, ukizifanya mtadumu.

(1) Kushukuru /Thanks You
Kwa kawaida wasichana huwa wanapenda sana kusikiliza maneno yanayotoka midomoni, mwa wapenzi wao. Hivyo kumfurahisha mpenzi wake, ni lazima kumshukuru kwa chochote atakachokufanyia kwa kusema hasante, hata kama ukimtuma akakuletee soda kwenye friji, au kitu chochote, hata kama alichokuletea si sahihi kumkosoa papo hapo ni bora kumshuruku na kumwambia taratibu.

KUWAPAMOJA / CROWD
Mwanamke anapenda sana kuongozana na mpenzi wake, anapenda kuona kila saa akiwa karibu na ampendaye. Inawezekana mkaongozana wakati wa starehe, kama kwenda beach, disko, kwenye harusi au kuongozana kwenda kazi, sokoni kama Supermakert , Kliniki wakati wa ujauzito au maradhi ya kawaida ni bora kufuatana. Wanasema kuongozana mara kwa mara kunafukuza maadui, kwani hakuna mtu anayeweza kuingiza chuki kwani hata yeye ataogopa.

KULALA / SLEEP
Najua kila wapenzi wanakitu ambacho wanakipenda pamoja. Japokuwa kati ya hao, wengi hupenda kutizama Tv, filamu. Kama mtakuwa mnaangalia filamu, ruhusu mwenzawako, alale kifuani kwako, au sehemu yoyote ya mwili wako.

Na pindi akipitiwa na usingizi usimwamshe, mwache alale hadi atakapoamka mwenyewe kwakuwa mwili pia unahitaji mapumziko. Kama kuna joto, iwe usiku au mchan, jitahidi umwache apitiwe na usingizi mwilini mwako, hii inasaidia sana kwani siku akilala peke yake, atajikuta akikukumbuka zaidi.

BUSU /KISSES
Wanasema busu au kiss huongeza ukaribu baina ya wapenzi. Hivyo penda kumkisi mpenzi wako, shavuni, kwenye paji la uso au mdomoni..

KUMVALISHA NGUO YAKO WAKATI WA BARIDI /JACKET
Ni vema kama kipindi cha baridi uonyeshe ni jinsi gani unamthamini, au unamfanya yeye kuwa kipaumbele zaidi kwako kwa kuchukua nguo yako, koti au shati na kumvisha au kumfunika.

Yeye kutumia nguo yako sehemu ambayo unahisi hamna kitu kingine cha kumfunikia au kumkinga na joto, au baridi, joto atakalo pata ni sawa na lile joto la mapenzi.


KUMSAIDIA KUOSHA VYOMBO/ WASHES
Jamani, sio ujinga kumsaidia mpenzi wako katika suala zima la usafi wa nyumbani. Muwe mlishinda wote nyumbani, au mmerudi wote kazini au safari . Kama mwenzako ataingia jikoni, akapika na kuandaa chakula, ni vema ukawa unamsaidia kwa kuandaa vitu vingine. Pia ni vema ukawa unasafisha chombo ulichotumia wewe au yeye kama grasi ya maji ya kunywa au kijiko, hii inamfanya aamini kama yeye si mtumwa kwako, na akumbuke wema wako popote aendapo.


KUMSIFIA / APPRICIETY
Unapokuwa na mpenzi wako penda kuchumnguza jinsi anavyovaa, anavyokula na chochote anachofanya. Siku ukiona ameongeza kitu cha ziada katika kile kitu cha kawaida basi msifie. Mwanamke au mwanaadam yoyote anapenda sifa, akipika wali nyama siku akiongeza na njegere mwambie, Chakula cha leo kitamu sana, akivaa nguo au akisuka mwambie mwambie umependeza. Basi atakupenda kwakuwa atahisi yeye ni bora zaidi ya hao unaokutana nao nje.


ZAWADI / GIFT
Jamani jamani!! Hebu nisikilizeni mimi, watu wanaogopa neno zawadi, zawadi si lazima mtu umpe nyumba au gari. Mpenzi wako anahitaji vizawadi, vidogo vidogo, kwa mfano kumnunulia ua la upendo, kumnunulia kadi, kumnunulia Bazoka, fenesi, embe, peasi, gauni, chungwa na kitu chochote ambacho unahisi unakimudu. Zawadi inaonyesha ni jinsi gani unavyoweza kushea kile ambacho unakipata, hivyo hatojali ukubwa wa zawadi na atathamini zaidi hali yako kwakuwa anajua ipo siku atapata kubwa huku uzee unasogea.

KUMKUMBATIA/ CUDDLING
Wanasayansi wanasema kumkumbatia mtu kunamsaidia kumpunguza mawazo, kwakuwa kunaonyesha ni jinsi gani unavyomthamani na hata kuonyesha unaweza kuwa sehemu ya suruhisho la tatizo lake. Hivyo ni vizuri kupenda kumkumbatia si kitandani pekee yake, bali iwe beach, kwenye kochi, ndani ya gari sehemu yoyote ambapo panastahiri kumkumbatia mkumbatie. Hebu chunguza, watu waliopoteana kwa muda mrefu na wanapokutana, angalia kwenye misiba na sehemu zingine. Penda kucheza naye kwa kukumbataiana utaona matokeo yake.

KUAGANA NA KUKARIBISHANA/ HELLO & GOODBYE
Kama asubuhi unaondoka kwenda sehemu yoyote penda kumuaga mpenzi wako kwa staili ambayo wewe unaipenda, kama utachagua ya kumkumbatia, kushikana mikono, au kufanya ishara yoyote, ingawa njia nzuri zaidi ni ya kupigana kisi. Mkisi mpenzi wako wakati unarudi kazini, au wakati wa kwenda kazini, ni njia bora ya kukumbuka popote unapoenda. Na kufanya hivyo utakuwa umeweka ulinzi katika penzi lako.


Jamani hapo ndiyo mwisho… kufanya hivi utakuwa umelilinda penzi lako.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.