HABARI NJEMA KUTOKA TIMU YA YANGA, YANGA HAWASHIKIKI

Image result for Yanga wakiwa uwanjani
Klabu ya Yanga kupitia kwa kwa katibu wake Mkuu Boniface Mkwasa amesema wako katika mchakato wa kujenga uwanja wao wa Kaunda uliopo makao makuu ya Klabu yao, Mkwasa amesema kama wanachama, wapenzi na wadau wa klabu hiyo wataungana na kuweka Nguvu ya Pamoja basi ni wazi mchakato huo utaenda kwa wakati.

Mkwasa amesema pia Kama mchakato huo Utaenda sawa basi wanampango wa Kuhakikisha mzunguko wa pili wa Ligi Kuu mechi zao zichezwe katika uwanja Huo.

Kuhusu Idadi ya watu Watakaokuwa na Uwezo wa Kukaa kwenye uwanja huo, Mkwasa amesema Uwanja wa Yanga utakuwa na uwezo wa Watu kati ya Elfu kumi na tano (15,000) Mpaka Elfu Ishirini (20,000).

Katibu Mkuu amesema watamwaga vifusi vya Kutosha ilikuinua eneo hilo ili kuepusha suala la Maji Kujaa hali ambayo inaweza kusababisha Mafuriko katika eneo hilo kama ambavyo mara kadhaa imekuwa Ikitokea.

Ishu hii inaonekana tayari mipango mingi ishaanza kunoga kwani siku kadhaa mmoja ya wajumbe wa Kamati ya utendaji bwana Salum Mkemi alipost picha Instagram akiwa na Mchina huku akiweka Caption ya Deal Done.

Yanga kabla ya Kuja na Mchakato wa Uwanja waKaunda walikuwa na Mipango kujenga uwanja wao Kigamboni eneo walilopewa na Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Zamani wa Klabu hiyo Yusuph Manji kabla ya Serikali kulichukua Eneo hilo siku chache zilizopita.

Baada ya serikali kulichukua eneo hilo watu wengi walijua itakuwa mwisho wa Yanga kuendelea na michakato ya uwanja lakini kuanza tena kwa mchakato huo kutawashtua wengi..

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.