HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA NAIROBI KENYA ANAKOTIBIWA MH. TUNDU LISSU


Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amesema wamefika salama Nairobi nchini Kenya na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea vizuri na matibabu.

Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mbunge Msigwa amewataka watu waendelee kumuombea Lissu aliyesafirishwa jana usiku kupelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Mawakili cha Kenya (LSK), Isaac Okero amesema wanachama wa Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki leo mchana wataenda kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).
Close Menu