CHEKI BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA ILI KUIMALIZA YANGA LEO


HATIMAYE kumepambazuka salama na hali ya hewa ikiwa inaruhusu kila kitu kitokee kama ambavyo kimepangwa.

Uwanja wa Mkapa saa 11:00 kunatarajiwa kuwa na burudani ya maana kwa timu mbili Bongo ambazo ni Simba v Yanga.

Watani hawa wa jadi wanakutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na hapa tunakuletea benchi la ufundi ambalo litakuwa na kazi ya kusaka Ngao ya Jamii kwa kutumia vijana wao uwanjani namna hii:-

BENCHI LA UFUNDI SIMBA
Kocha Mkuu wa Simba ni Didier Gomes (Ufaransa), makocha wasaidizi; Seleman Matola (Tanzania) na Thierry Hitimana (Rwanda), Kocha wa makipa ni Milton Mendv (Brazil).

Kocha wa utimamu wa mwili ni, Adel Zrane (Tunisia), Meneja wa timu: Patrick Rweyemamu, Mchua Misuli: Jallow Bakari, daktari wa timu ni Yassin Gembe na mtunza vifaa ni Hamis Mtambo wote wa Tanzania na Fareed Cassiem wa Afrika Kusini.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.