LULU AMJIA JUU WEMA SEPETU, ATEMA NYONGO KWA HASIRA

Kimeumana ile mbaya! Kwa mara ya kwanza, baada ya kusambaa kwa ubuyu kwamba ana ugomvi na staa mwenzake wa Bongo Movies, Wema Sepetu, Elizabeth Michael au Lulu amevunja ukimya.

Kabla ya Lulu kufunguka kilichomkwaza kwa Wema, ilisemekana kwamba, Wema alimtaja Lulu kwenye kipindi chake cha Cook With Wema Sepetu ambapo alimuita Mama Kanumba na kumuuliza juu ya kifo cha Kanumba na mambo ya Lulu.

Jambo hilo lilisemekana kumkwaza Lulu na kuvunjika kwa amani kati yake na Wema kiasi cha kuondoana kwenye ufuasi (un-follow) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kwamba hakutakuwa tena na urafiki wa wawili hao.

Lulu amesema; “Kiukweli mimi na yeye sioni kama kuna kitu cha kumaliza, yeye aliongea kile ambacho aliona kinastahili kuongeleka.

“Mimi kukereka ni reaction (mapokeo) yangu. Unajua kwenye maisha tunafanya vitu na kinavyopokelewa na mtu ni maamuzi ya mwingine. Yaani wewe unaweza ukafanya kitu ili kumpendezesha mtu f’lani kumbe yeye mapekezi yake hakimpendezeshi badala yake kinamkwaza. Mimi naamini pengine yeye aliona kipo sawa, lakini kwenye mapokezi yangu mimi sikuona kipo sawa.”

Itakumbukwa kwamba, Wema na Lulu walishakuwa wachumba wa Kanumba kabla ya kutangulia mbele za haki siku ile ya Aprili 7, 2012.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu