NEYMAR JR AFIKIRIA KUSTAAFU

NYOTA wa timu ya taifa, Neymar Jr ameweka wazi kwamba baada ya kucheza Kombe la Dunia lijalo la mwaka 2022 hajui kama akili yake itakuwa tayari kuendelea kupambana kwenye soka au laa.

Kauli hiyo inaamanisha kwamba huenda baada ya kukamilika kwa Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar staa huyo anaweza kustaafu masuala ya mpira.

Brazil kwa sasa inapambania tiketi ya kuweza kufuzu Kombe la Dunia na nyota huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya PSG aliweza pia kuwa kwenye kikosi kilichonyooshwa mabao 7-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Staa huyo amesema kuwa kombe la dunia la mwakani ndilo litakuwa la mwisho kwake kucheza kwa sababu hajui baada ya hapo atakuwa tayari kuendelea kucheza.

"Nafikiri Kombe la Dunia lijalo litakuwa la mwisho kwangu, nahisi itakuwa hivyo kwa sababu sijui kama nitakuwa tayari kuendelea kucheza na sijui akili yangu itakuwa tayari kuendelea kupambana ama laa," .
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.