SALAH,MESSI NA VINICIUS JUNIOR WANG'AA KATIKA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA

Mohamed Salah aliendelea kudhirisha hali yake bora ya mchezo kwa kufunga mabao mawili katika mchuano wa ligi ya mabingwa wa makundi ulioifanya Liverpool kuishinda Athletico Madrid mabao matatu kwa mawili na kufanikisha ushindi wa mechi zao tatu za makundi .

The Reds hata hivyo ilijionea kioja baada ya mabao yao mawili ya kwanza kufutwa na mawili ya Antoine Griezmann.Mfaransa huyo kisha alionyesha kadi nyekundu katika kipindi cha pili hatua iliyowawezesha wageni kuonyesha makali yao na kufunga bao la ushindi kupitia Penalti ya Salah

Lionel Messi alifunga mabao mawili katika mchuano ambao Paris St-Germain ilitoka nyuma na kuichabanga RB Leipzig mabao matatu kwa mawili katika mcvhuano wa Champions League.

Kylian Mbappe aliwaweka wageni kifua mbele lakini Andre Silva ana Nordi Mukiele walifunga kupitia pasi za Angelino kuwaweka wajerumani hao kifua mbele

PSG ilipata penalti dakika za mwisho mwisho za mechi hiyo lakini badala ya Messi kuipia Mbappe aliifyatua juu ya lango

Vinicius Junior alifunga mabao mawili katika ushindi wa Real madrid wa mabao matano kwa nunge dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mchuano wa Champions League.

Bao la kujifunga wenyewe la Sergiy Kryvtsov liliipa Real uongozi wakati wa kipindi cha mapumziko.

Katika mechi nyingine za ligi ya mabingwa zilizosakatwa jana,Manchester City iliishinda Club briges mabao matano kwa moja ,Sporting Lisbon ikaizaba Beskitas mabao manne kwa moja,FC porto ikapata ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya AC Milan ,Ajax ikaiadhibu B.Dortmund mabao manne kwa nunge nayo Inter Milan ikaizaba Sheriff Tiraspol mabao matatu kwa moja.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu