YANGA KUWEKA KAMBI ARUSHA


Baada ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Geita Gold kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema timu hiyo itaweka kambi Arusha katika muda wa mapumziko kupisha kalenda ya mechi za Fifa.

Nabi amesema muda huo atautumia kurekebisha makosa aliyoyaona katika michezo iliyocheza Yanga kwa hivi karibuni.

“Natambua timu yangu bado haijawa sawa ila nimefurahia ushindi, kwa muda ambao ligi itasimama kupisha kalenda ya Fifa timu haitapumzika bali tutaelekea Arusha kuendelea na maandalizi ya mechi zijazo” anasema kocha Nabi.

Yanga imeshinda mechi zake zote mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo mechi ya kwanza walishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na jana wakishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.