https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d CV YA KOCHA MPYA WA VIUNGO WA SIMBA NI BALAA - MASENGWA BLOG

CV YA KOCHA MPYA WA VIUNGO WA SIMBA NI BALAA

UJIO wa Kocha mpya wa viungo wa Simba, Don Daniel De Castro sio habari kubwa sana mjini kama ilivyokuwa kwa kocha mkuu Pablo Franco, ila kwa wasifu ni wazi Wekundu wa Msimbazi wamelamba dume.

Castro ambaye amekuja kuziba nafasi ya Adel Zrane raia wa Tunisia aliyeachana naye hivi karibuni, ana digrii ya Physical Fitness Training aliyoipata Chuo cha Real Madrid na amewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya miaka 18 ya Real Madrid msimu wa 2018/19.

Costro alihusika kuwatengeneza nyota kama Carlos Algarra anayechezea Cadiz, Sergio Lopez aliyepo FC Basel, Cesar Gelabert anayeitumikia Milandes na Fran Garcia aliyepo Rayo Vallecano.

Msimu wa 2019/20, alikuwa kocha msaidizi wa viungo wa timu ya Rapid Bucharest ya Romania na 2020/21 alikuwa kocha msaidizi wa viungo wa Politehnica Ias ya Romania.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema walitoa nafasi ya makocha kutuma maombi na CV iliyoangaliwa na kupitishwa ni ya kocha huyo kwani walivutiwa nayo.

“Suala la mkataba wa muda gani hilo ni baina yetu na mwajiriwa, kuhusu kocha huyo kupendekezwa na Pablo hapana, ni maombi yalitolewa na tumemchukua kutokana na kuwa na wasifu mzuri,” alisema Mangungu.

Kocha huyo aliwasili jijini Dar es Salaam mapema juzi na jana alianza kazi akiungana na Pablo aliyejiunga na timu hiyo wiki iliyopita.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.