080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d HAJI MANARA AWAVURUGA SIMBA KUHUSU CHAMA, ADAI BIASHARA WALISHAMALIZA - MASENGWA BLOG

HAJI MANARA AWAVURUGA SIMBA KUHUSU CHAMA, ADAI BIASHARA WALISHAMALIZA

Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa klabu yake imeshamaliza biashara kwa mchezaji mmoja mkubwa wa kimataifa na viongozi wa klabu hiyo kwa sasa wanashungulikia ICT (hati ya uhamisho).

Katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa Instagram Manara ameweka wazi kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni kutangazwa rasmi kwa mchezaji huyo.

"Nchi tuisimamishe sasa hv au baadae? Dadadeki, Ok biashara tushamaliza na hapa Hersi @caamil_88 ndio anashughulikia ATC, oooh Tholi ni ITC, Jana mliongopewa nn vile?, We Are Yanga, The Home of Champions, Sijui nifanye Press au niseme humu humu, halaf wala haturingi" ameandika Haji

Kwa muda mrefu sasa klabu ya Yanga imekuwa ikitajwa kufanya usajili wa kiungo Clatous Chama anayecheza kwenye klabu ya RS Berkane huko Morocco.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.