HII MPYA, AUCHO BILA KUPEPESA MACHO AMPA NENO ZITO FEISAL TOTO

KIUNGO wa kati wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho, amesema kiungo mwenzake, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ana balaa, huku akiweka wazi namna anavyokoshwa na mabao ya mbali anayoyafunga.

Aucho ambaye amejiunga na Yanga msimu huu, amekuwa mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo akiingia moja kwa moja kikosi cha kwanza akicheza sambamba na Yannick Bangala Litombo raia wa DR Congo.

Katika mechi tano ambazo Yanga imecheza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, Mganda huyo amecheza nne, akikosekana dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Yanga ilishinda 3-1.

Akizungumza Aucho alisema: “Mabao ya Feisal yamenivutia, yanayostahili kufungwa na mchezaji anayecheza katika eneo lake.

“Ukiachana na kufunga mara kwa mara, ni nadra kuona wachezaji katika eneo lake wakifunga kama yeye, ilikuwa katika kizazi cha zamani lakini Feisal yeye anafanya katika kizazi hiki. Anafanya mambo makubwa sana.

“Lakini mbali na yote hayo, ameisadia timu kupata ushindi katika michezo miwili kwa aina yake ya mabao, kwetu kama wachezaji tunafurahi kuona hilo. Malengo ya timu ni kupata ushindi katika michezo yetu, utekelezaji unakuja kutokana na kujituma kwetu.”

Fei Toto mwenye mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, mawili aliyafunga kwa mashuti ya mbali dhidi ya KMC na Ruvu Shooting.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.