KOCHA APIGWA RISASI MECHI IKIENDELEA UWANJANI, MECHI ILIKUWA BALAA

WACHEZAJI walilazimika kukimbia dimbani wakati mashabiki wa Klabu ya Hurucan Las Heras walipokuwa wakicheza dhidi ya Ferro de General Pico katika ligi ya kijimbo.

Kanda za video zilionesha wachezaji wa timu zote mbili wakikimbilia kujificha wakati risasi zilipofyatuliwa ndani ya uwanja huo uliopo mkoa wa Mendoza ambapo Kocha wa Ferro, Mauricio Romero alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Romero kwa sasa anaendelea vyema na hayuko hatarini" , klabu ya Ferro ilisema katika taarifa yake katika mtandao wa twitter. Baada ya kuondoka uwanjani, alifanyiwa vipimo katika hospitali moja na baadaye kutoa taarifa kwa polisi.

Mechi hiyo ilisitishwa baadaye katika kipindi cha pili wakati walipokuwa wakiongoza 3-1 na Huracan imekosoa wale waliohusika katika tukio hilo. Mkufunzi mmoja wa kandanda alipigwa risasi katika bega wakati wa mechi ya daraja la tatu nchini Argentina siku ya Jumapili.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu