https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d CHAMA ALIAMSHA DUDE HUKO MOROGORO, KILA MMOJA ADUWAZWA - MASENGWA BLOG

CHAMA ALIAMSHA DUDE HUKO MOROGORO, KILA MMOJA ADUWAZWA


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama ameanza kuwapa raha mashabiki wake mapema baada ya kupiga pasi zinazofika eneo husika.

Kocha wa Simba, Pablo Franco aliwapanga Chama, Rally Bwalya na Bernard Morrison kupiga mashuti nje ya 18, pia kupika kona.

Chama alifikisha mashuti yake eneo linalotakiwa, jambo ambalo liliwapa raha mastaa wenzake.

Pablo ni kama anamkabidhi majukumu Chama ya kupiga faulo, kwani amewatenga pembezoni mwa uwanja kupiga faulo, akiwa na Bwalya.

Kwa namna kocha anavyompa majukumu Chama ni dhahiri atampanga mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao utapigwa Manungu.

Chama alipiga shuti kwa Hassan Dilunga ambaye alitokea katikakati la kundi la wachezaji wengine, huku Meddie Kagere,Chris Mugalu na Sakho wakikimbia kufunga.ADVERTISEMENT


Amewatenga mabeki Joash Onyango,Juma Kennedy na Inonga kuwawahi kina Kagere mbele.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.