https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d KISA KIPIGO KUTOKA MBEYA CITY...PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA..AFUNGUKA ALIYOTARAJIA...AWATAJA WACHEZAJI.. - MASENGWA BLOG

KISA KIPIGO KUTOKA MBEYA CITY...PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA..AFUNGUKA ALIYOTARAJIA...AWATAJA WACHEZAJI..

KIPIGO ilichopewa Simba na Mbeya City kimemzindua kocha Pablo Franco aliyekiri wapinzani wao waliwazidi ujanja, ila wamejipanga upya ili kutorudia tena makosa katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ikiwamo ya wikiendi hii.

Simba ilifungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na wenyeji wao ikiwa ni kipindi cha kwanza msimu huu katika ligi, huku Pablo akikiri City ilikuwa bora kuliko wao licha ya kucheza pungufu na sasa wanajipanga upya.

“Tulijua mchezo ungekuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu. Hatukupata muda wa maandalizi zaidi baada ya kutoka michuano ya Mapinduzi. Pia uwanja nao haukuwa rafiki kwa upande wetu,” alisema Pablo.

“Wachezaji wangu walijitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata matokeo, ilibidi tubadili mfumo baada ya City kuwa pungufu ila haikusaidia.”

Alisema kwa sasa wanajipanga upya kwa ajili ya mechi zao zijazo ukiwamo wa Jumamosi ya kesho watakaovaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Pablo alisema asingependa kuona wanapoteza pointi nyingine zaidi, kwa itawapa ugumu kufukuzana na watani wao, Yanga wanaoongoza msimamo kwa sasa kwa tofauti na pointi nane licha ya wao kucheza mchi 12, moja zaidi na ile ya Simba.

Naye mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo, Ahmed Ally alisema matokeo ya Mbeya City yamewafanya kuchukua tahadhari katika kila mchezo uliopo mbeleni ili waweze kufikia malengo.

“Matokeo ya Mbeya yametufanya kuchukua tahadhari katika kila mchezo uliopo mbele yetu, hivyo mashabiki wetu watarajie mabadiliko yatakayoambatana na ushindi,” alisema.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.