KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...MTIBWA WAHAMISHIA MECHI UWANJA AMBAO SIMBA WALIFUNGWA GOLI 3..

KAMA mashabiki wa Simba, walijipanga kwenda kuangalia timu yao ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri mambo yamebadilika badala yake itapigwa Manungu.

Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar, Abubakar Nassor amethibitisha jambo hilo, kwamba mechi hiyo itapigwa uwanja wa Manungo, mkoani Morogoro.

Amesema uwanja huo umekamilika, hivyo wanaona ni wakati sahihi wa kuanza kuufanyia kazi na wanaanza kucheza dhidi ya Simba.

"Uwanja wetu wa Manungu tumeufanyia ukarabati, hivyo mechi yetu na Simba itachezwa uko,"amesema Nassor na ameongeza kuwa;

"Mashabiki wetu wajiandae kuangalia ama kuisapoti timu yao kwenye uwanja wao, tunategemea watafurahia jambo hilo,"amesema.

Mechi hiyo, imatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi (Januari 22, 2022), huku wenyeji wao Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa nje, ndani kwa jumla ya mabao 6-2.

Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 20, ambapo mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye uwanja huo, mechi ilivunjika mara baada ya Simba kugoma kuendelea na mechi ambapo katika kipindi cha kwanza tu walikuwa wameshanyukwa goli tatu bila.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu