https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d MO DEWJI ACHARUKA... NI KUHUSU USAJILI MPYA NDANI YA SIMBA...BAADHI YA WACHEZAJI AWAKATAA...AMTAJA CHAMA - MASENGWA BLOG

MO DEWJI ACHARUKA... NI KUHUSU USAJILI MPYA NDANI YA SIMBA...BAADHI YA WACHEZAJI AWAKATAA...AMTAJA CHAMA

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema klabu hiyo imefunga usajili wao msimu huu.

Amesema watamtambulisha nyota mpya kutoka nje ya nchi ambaye ndiye amewafungia usajili wao wakati huu wa dirisha dogo.

"Tayari tumekwishamaliza naye, ila sitomtaja jina na nchi anayotoka sababu utamfahamu, lakini tumemalizana naye na hivi karibuni atatambulishwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Try Again (Salim Abdallah)," amesema Dewji.

Hivi karibuni Simba kwenye mkutano mkuu ilifichua kuwa na mpango wa kumrejesha Cleotus Chama.

Katika hotuba yake, Try Again alisema watamrejesha mchezaji huyo jambo ambalo lilishangiliwa na mamia ya wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam.

Kuhusu wachezaji waliokuja nchini kwa ajili ya majaribio kwenye timu hiyo, Kassim Dewji amesema hakuna hata mmoja atakayesajiliwa na klabu hiyo msimu huu.

"Mawakala wao ndiyo waliomba waje kufanya majaribio, kama klabu hatukuona sababu ya kuwakatalia, lakini kama nilivyosema hakuna hata mmoja ambaye atasajiliwa kati yao kwenye timu yetu," amesema.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.