https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d UGONJWA WA KORONA WASALIMU AMRI AFRIKA, WHO WASEMA HAYA... - MASENGWA BLOG

UGONJWA WA KORONA WASALIMU AMRI AFRIKA, WHO WASEMA HAYA...

Kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa mlipuko wa virusi vya Omicron, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema idadi ya maambukizi mapya ya COVID-19 Afrika imepungua na hivyo basi kuleta matumaini miongoni mwa Wanasayansi.

“Ni habari njema kuona maambukizi ya ugongwa huo yanapungua, nadhani ni bayana na kuna ishara kwamba idadi ya maambukizi kutokana na wimbi la nne la COVID-19 imepungua sio tu nchini Afrika Kusini bali pia kote Barani Afrika, ukiondoa maambukizi mapya tunayoyashuhudia kwenye baadhi ya Nchi za Afrika ya Kaskazini zinazokabiliwa na majira ya baridi kali”.

Watalaamu kutoka WHO wamedokeza kuwa idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona barani Afrika imepungua kwa asilimia 8 na kusema wimbi la nne la Covid-19 limefika kileleni Afrika “japo makali ya wimbi la sasa yanaonekana kufifia, Bara la Afrika bado halijaondokana na janga la COVID-19 , Serikali za Nchi za Afrika zisilegeze kamba”
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.