Breaking News : MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA
Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa Ikulu ni mwendelezo wa kikao cha Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichofanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa ya wataalamu kuhusu nyongeza ya mishahara.
Nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi.
Kutokana na hatua hiyo katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.
Hivyo bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 ina ongezeko la Shilingi trilioni 1.59 sawa na 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22.
Wakati huo huo, Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya Mafao ya Pensheni kama Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) lilivyoomba Mei mosi, 2022.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: