BREAKING: SIMBA SC YAMTEMA MORRISON
Klabu ya Simba imempa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji wake Bernard Morrison raia wa Ghana.
Taarifa ya Simba imeeleza kuwa I mefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.
Aidha Klabu hiyo imetoa shukrani kwa Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu hiyo.
“Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kuisadia kupata mafaniko kadhaa ikiwemo kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam Sports, na ubingwa wa kombe la Mapinduzi,” Taarifa ya Simba
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: