HIZI HAPA POINTI ALIZOBAKIZA YANGA AKABIDHIWE UBINGWA...


YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanya kubakiza alama sita pekee ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 63 baada ya mechi 25 za Ligi huku ikihitaji alama sita kwenye mechi tano zilizobaki ili kuwa bingwa kwani itafikisha jumla ya pointi 69 ambazo hakuna timu yeyote itazifikisha baada ya mechi zote kumalizika.

Pia ushindi huo umeifanya Yanga kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi kwenye Ligi msimu huu ikiwa imecheza 25 kushinda 19 na sare sita.

Wakati Yanga ikichekelea na ushindi huo, hali si shwari kwa Mbeya Kwanza kwani imeendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa Ligi na alama zake 21 ikiwa imebaki na mechi tano tu.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu