https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d MBOWE AWATAKA VIONGOZI WA CHADEMA KUHESHIMU VYAMA VINGINE...CCM NA CHADEMA KUKUTANA WIKI IJAYO - MASENGWA BLOG

MBOWE AWATAKA VIONGOZI WA CHADEMA KUHESHIMU VYAMA VINGINE...CCM NA CHADEMA KUKUTANA WIKI IJAYO

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe amewataka viongozi wa CHADEMA kuheshimu vyama vya siasa vingine huku akiwatahadharisha wale walio ndani au nje ya CHADEMA watakaoihujumu CHADEMA.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Mei 11, 2022 CHADEMA wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam lililohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Tusipoteze muda kujadili wengine, tutumie muda mwingi kujenga CHADEMA. Lazima tuheshimu vyama vingine vya siasa kwa sababu hujui kesho chama kipi kitakuwa chama kikuu cha upinzani. Tusiwe wepesi wa kushambulia wenzetu kwa sababu huwezi jua huenda uwezo wao umeishia hapo",amesema Mbowe.

"Wiki ijayo tutaanza vikao vya CHADEMA na CCM Tumepanga kukutana Delegation ya CHADEMA yenye wajumbe wasiozidi 10 na Delegation ya CCM wiki inayokuja, tutaenda kuzungumza nini kinafanya taifa letu lisiende mbele. Tunataka kutengeneza mahusiano ya msingi. Watu wetu wamekuwa na hofu kwa sababu ya kutoaminiana. Tunataka kujenga taifa",ameongeza Mbowe.

Aidha amezitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuheshimu Demokrasia bora.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.