MBUNGE ADAIWA KUGUSHI VYETI VYA SHULE


Mbunge wa Kenya ambaye anatuhumiwa kughushi vyeti anadaiwa kuwa hakufanya mitihani yake ya mwisho katika shule ya upili anayodai kuwa alisoma, mwalimu wa zamani shule ameambia mahakama.

Mbunge huyo, Oscar Sudi, alisema kwamba alifanya mitihani hiyo katika Shule ya Sekondari ya Highway mwaka wa 2006. Lakini mkuu wa zamani wa shule hiyo alisema nambari ambayo Bw Sudi alisema ilikuwa yake ni ya mwanafunzi mwingine, na kuongeza kuwa mbunge huyo hakujisajili wala kufanya mtihani shuleni.

Mbunge huyo ameshtakiwa kwa kughushi cheti cha stashahada na cheti cha shule ya upili. Lakini Amekanusha mashtaka na yuko nje kwa dhamana.

Kulingana na gazeti la Standard la Kenya, madai hayo ya kughushi yalianza tangu alipokuwa akitafuta kibali cha uchaguzi mwaka wa 2013 ambapo sheria iliwataka wagombea ubunge kuonyesha uthibitisho wa elimu ya baada ya sekondari.

Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu