https://www.trustedcpmrevenue.com/h5yiguxem?key=39c4c47214b00b0a7509b8ad7d241932080dff1c1eecb0b9da6cc290262c1e4d WABUNGE 19 WALIOFUKUZWA CHADEMA WAFUNGUKA... HALIMA MDEE ASEMA KILICHOFANYIKA NI UHUNI MTUPU...MBOWE AJIBU UHUNI WAO - MASENGWA BLOG

WABUNGE 19 WALIOFUKUZWA CHADEMA WAFUNGUKA... HALIMA MDEE ASEMA KILICHOFANYIKA NI UHUNI MTUPU...MBOWE AJIBU UHUNI WAO

Baraza kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limetupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama wake 19 na kubariki maamuzi ya kuwafukuza uanachama yaliyofanywa na Kamati kuu ya chama hicho mwaka 2020.

Maamuzi hayo yamefikiwa usiku huu Mei 12,2022 kwenye kikao cha Baraza Kuu kilichoanza kufanyika Mei 11,2022 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baada ya maamuzi hayo, Mbunge Halima Mdee kwa niaba ya wenzake 18 ameelezea kutokubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wa kutupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chama hicho akisema kilichofanyika ni uhuni.

"Nakwepa kuzungumza maneno makali kwa sababu naheshimu viongozi wangu lakini sikujua CHADEMA umeanza kufanyika uhuni kwa kiwango hicho, Mimi ni CHADEMA naendelea kuwa CHADEMA lakini kilichofanyika pale ni uhuni wa kiwango cha hatari , nitaongea siku nyingine lakini kilichofanyika pale hata Mbowe anajua ni uhuni",amesema Mdee.

Mdee ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe na wenzake 18 wamefukuzwa Chadema baada ya Baraza Kuu CHADEMA kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.