AFARIKI AKISHANGILIA GOLI LA PILI LA MAYELE MECHI YA NGAO YA JAMIIKatika hali ya kusikitisha, shabiki mmoja wa Klabu ya Yanga aliyetambulika kwa jina la Leonard John mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amefariki dunia kufuatia furaha ya goli la pili la Mayele akiwa anaangalia mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa siku ya tarehe 13/08/2022 kati ya Yanga na Simba ambapo Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Simba.

Kutokana na furaha ya bao la pili la ushindi la Yanga lililofungwa na Fiston Mayele akiwa katika kibanda cha kuangalizia mpira Kimara jijini Dar es Salaam, marehemu alijawa na furaha iliyopelekea kukutwa na umauti papo hapo

Rafiki yake wa karibu Laurent Macharo ameeleza kuwa katika ile furaha kulishangilia la Mayele baada ya kufunga lile goli la ushindi ambao dakika zilikuwa zimeshaenda za lala salama, Bwana Leonard alinyanyuka na kuruka juu kushangilia ghafla Bwana Leonard aliteremka taratibu mpaka chini na kupiga magoti na kuanguka na hakuweza kuongea tena" Alisema Laurent

Laurent aliongeza kuwa walimkimbiza katika zahanati ya jirani kwa ajili ya kujaribu kuokoa uhai wake lakini walipomfikisha tayari alikuwa ameshafariki

Marehemu Leonard John ameacha watoto wawili na mke, huku wadau na majirani wakiomba msaada kutoka katika klabu ya yanga kupitia Rais Heris kusaidia kuratibu mazishi na kuweza kusafirisha mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi mkoani Manyara.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.