BERNARD MORRISON AZUA JAMBO HUKO YANGA, WACHEZAJI WENZAKE WACHEKA HADI MACHOZI


Kama ulikuwa unadhani BM33 kabadilika kwa vituko pole yako, kwani jamaa baada ya kings na wachezaji wenzake yanga amegeuka gumzo kwa wachezaji wenzake wakati wa utambulisho na kusababisha Nabi kupigwa butwaa.

Ipo hivi. Wakati wa utambulisho wa wachezaji wapya ilipofika zamu ya Morrison, kocha Nabi alimtaka ajitambulishe ndipo akafanya timu nzima iangue kicheko.

Morrison akiwa uso mkavu alimjibu Nabi; “Jamani... jamani kocha ujitambulishe wewe, mimi ni mwenyeji hapa.” Jambo ambalo lilimfanya Nabi ashindwe uvumilivu na kuangua kicheko.

Wakati kocha Nabi anaendelea kucheka, Morrison aliendelea na utani wake kwa kuwauliza wachezaji aliocheza nao kabla ya kuhamia Simba alikocheza 2020-2022.

“Nyie mliokuwepo eti hamnifahamu jamani...jamani, wewe Fei Toto na wewe hunifahamu.” Jambo lililofanya timu nzima wacheke wakishindwa kuvumilia kuendelea kumsikiliza.

Hata hivyo, ilimlazimu kocha amwambie apunguze utani na ajitambulishe kisha waendelee na mazoezi na akafanya hivyo.

Wachezaji wa timu hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema hadi sasa mchezaji anayeongoza kwa ucheshi na vituko huko kambini ni Morrison anayejichanganya na kila anayemuona mbele yake.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.