RAIS SAMIA AMPA NENO LA WIKI ALBERT CHALAMILA AKIWAAPISHA WAKUU WA MIKOA

Rais Samia Suluhu Hassan na Albert Chalamila (kulia).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila atulize akili na kwenda kumsaidia kufanya kazi katika eneo alilompangia.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 1,2022 wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa aliowaapisha hivi karibuni.

"Mwanangu Chalamila mategemeo yangu umekua sasa, akili imetulia wewe ni mfanyakazi mzuri lakini mtundu mno, sasa nilikuacha nje kidogo kipindi hicho nimeamua kukurudisha naomba ukakue,ukue akili itulie uende ukafanye kazi ukanisaidie eneo ulilopangiwa na hii haina maana kwamba umemaliza ukikaa umekaa, nakuangalia kwa ukaribu sana",amesema Rais Samia.

Hivi karibuni Rais Samia alimteua Albert Chalamila kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera baada ya kutengua uteuzi wake akiwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Juni 11,2021.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.