
Kampuni ya kubashiri ya m-bet imemwaga mabilioni ya fedha katika klabu ya Simba ikiwa ni mkataba wa miaka mitano kati ya kampuni hiyo na klabu ya Simba.
Akieleza katika mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya m-bet Allen Munshi ameeleza kuwa wameingia mkataba na klabu wenye thamani ya Tsh. 26, 168,005,000/= (Bilioni ishirini na sita milioni mia moja sitini na nane na elfu tano tu).
Allen Mushi ametoa mchanganuoa wa fedha hizo zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka hadi miaka mitano ikamilike.
“Mwaka wa kwanza – Bil 4.670
Mwaka wa pili – Bil 4.925
Mwaka wa tatu – Bil 5.205
Mwaka wa nne – Bil 5.514
Mwaka wa tano – Bil 5.853
Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally mesema hii pesa iliyotajwa haijahusisha malupulupu mengine ambayo Simba itayapata kutoka M-Bet.
“Leo ni siku kubwa kwa Simba na M-Bet. Swali kubwa ni kwanini M-Bet. Sababu kubwa ni wameweza kukidhi mahitaji yetu.”
“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania.”
Naye mtendaji mkuu wa Simba Barbra amesema kuwa hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake.
“Leo ni siku ya kuzungumza fedha. Kampuni kubwa hudhamini klabu kubwa.”