Kocha wa Yanga Professor Mohamed Nasreddine Nabi amewatoa hofu mashabiki na wanachama wote wa Yanga kuwa hana mpango wa kuondoka Yanga kwa sasa.
Bado nina malengo ya muda mrefu sana hapa Yanga,,najua msimu uliopita hatukufanya vizuri kimataifa lakini moja ya malengo yetu Kama Yanga ni kuona msimu huu tunafika mbali na nataka niwe kocha ambaye nitakwenda kuivusha salama kimataifa Yanga na walimu wenzangu,, Viongozi na mashabiki wetu wote wa Yanga
Tulikuwa na msimu mzuri sana msimu uliopita kwa kushinda mataji yote ya ndani,,hivyo nataka kwenda kuendelea na Yanga kwa miaka mingi ijayo kwa kushinda mataji makubwa sasa.