WACHUMBA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI ARUSHA

Simanzi zimetawala katika jiji la Arusha kufuatia vifo vya vijana wawili waliokuwa wachumba Esto na Nice Mawala mwenye umri wa miaka 24 waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la kwa Mrefu jijini humo.
Wawili hao inasemekana wote ni watoto wa matajiri wawili jijini Arusha wanaoishi Njiro wamepata ajali hiyo mbaya majira ya saa saba usiku wa Julai 30, 2022 baada ya gari waliyokuwa wakisafiri nayo aina ya Range Rover kupata ajali mbaya usiku huo na kusababisha majeraha makubwa yaliyopelekea umauti kuwakuta.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: