WAKATI SINGIDA BIG STARS WAKIKOMAA KUMUACHIA MBRAZILI KWA YANGA...NABI KAONA ISIWE TABU..KAAMUA KUTUMIA NJIA HII...

KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi amekiangalia kikosi chake na kukiri kama ataulizwa na mabosi wake ni staa gani anatamani kumwongeza kwa dharura basi ni winga mmoja tu. Mbrazili, Dario Frederico wa Singida Stars.

Nabi alisema amemwona Dario katika moja ya michezo ya timu yake na kutamani ubora wake na ametamka yuko tayari kuangalia upya juu ya nafasi ya Mbrazil huyo katika kikosi chake.

Ingawa Nabi ameonyesha tamaa hiyo tayari Yanga imeshakamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaohitajika kikanuni na kama akimpata atalazimika kumpunguza mchezaji mmoja.

Dario ana mkataba wa miaka mitatu na Singida na awali ulienea uvumi kuna harakati za Yanga kutaka kumsajili winga huyo.

“Nimemwona, kwanza niseme naiheshimu Singida kwa kuwa wana mkataba naye, kama viongozi wangu wakiniuliza sasa ni mchezaji gani tukuongezee, ningemtaja huyo (Dario) kwa haraka,” alisema Nabi.

“Ni winga bora sana anajua kucheza kisasa na kupangua ukuta, ninaye mtu bora kama huyo, lakini sio mbaya ukiwa na watu kama hao wawili.”

Yanga kama itamhitaji Dario kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika italazimika pia kulipa faini CAF kukamilisha usajili wake baada ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 15, 2022.

Kocha huyo aliongeza ubora wa Dario ulikuwa kitu mwafaka kwa timu yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika na wanahitaji watu walio bora katika kuleta matokeo ya haraka.

Wakati Nabi akiyasema hayo ingawa uongozi wa klabu yake umekuwa kimya kuzungumzia dili hilo, Mwanaspoti linafahamu mabosi wa Yanga walikuwa katika mazungumzo na wamiliki wa Singida ya kubadilishana wachezaji ili kumshusha Dario.

Hata hivyo, dili hilo limekuwa gumu kukamilika baada ya kuibuka kwa mgawanyiko ndani ya Singida na baadhi wamekuwa wakiweka ngumu wakitaka kumwona Mbrazil huyo anasalia katika timu yao.

Singida wamesisitiza hawako tayari kumuachia staa huyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.