HUYU HAPA MWAMUZI WA KIKE…ALIYEANDIKA REKODI YA HATARI…KARIAKOO DABI

Jonesia Rukyaa ndiye mwamuzi wa kwanza kuchezesha derby mbili ndani ya siku 25 katika msimu mmoja huku mmoja ukichezwa Uwanja wa Uhuru na mwingine Benjamini Mkapa.

Mchezo wa kwanza kati ya Simba Queens na Yanga Princess katika Ligi Kuu ya Wanawake na ulifanyika katika uwanja wa Uhuru, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na mfungaji wa mchezo huo kwa upande wa Simba ambao ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao Kupitia Jentrix Shikangwa kabla ya Wogu Chioma kuisawazishia Yanga Princess.

Mchezo wa pili uliofanyika Aprili 16 uliowakutanisha vidume wawili huku Simba wakianza kuwafunga Yanga dakika za mwanzoni kabisa bao lililofungwa na beki Henock Inonga na dakika ya 32 Kibu Denis kuwapa wekundu wa Msimbazi bao la pili.

Mchezo uliomalizika kwa matokeo ya 2-0 huku ukitengeneza historia mpya kwa Simba kuwafunga mara 32 watani wao tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Bara Mwaka 1965.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0753 336 000

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.