Zitto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ametoa msimamo wa kujiuzulu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na Twitter.
“Serikali ya CCM ikinionesha tani 1.5 milioni za chakula ambazo inataka kusambaza, najiuzulu Ubunge mara moja. Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu kwenye maghala yote ya NFRA.
“Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu,” ameandika Zitto.
Jana Waziri Mkuu Majaliwa Kassim aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kuna akiba ya chakula inayofikia tani 1.5 milioni ambazo tayari wameruhusu zisambazwe katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuuzwa katika maeneo mbalimbali na kudhibiti kupanda kwa bei.