![]() |
*Kuboresha mmeng'enyo wa Chakula:- Embe limebeba nyuzinyuzi{Fibers} ambazo kusaidia kusaga chakula mwilini.
*Kuboresha ngozi:-Embe imebeba Vitamin A, ambayo husaidia kupambana na mapele au chunusi. Ni moja ya Tunda zuri sana kutumia kwa kuboresha ngozi yako. Vitamin C na E iliyopo kwenye Embe hulinda ngozi na miale ya jua, inayoweza kuharibu ngozi yako.
Waweza chukua Embe lililoiva, lisage, kisha paka moja kwa moja kwenye ngozi yako kwa ajili ya kusafisha uso wako na uchafu ambao haundoki na sabuni pekee, na pia itakusaidia kufungua vijitundu vya ngozi.
*Kuboresha Kuona:- Embe imebeba Vitamini A yakutosha ambayo husaidia kuona. Hulinda jicho na matatizo yakutokuona mchana au usiku.
*Kuboresha Hisia za kimapenzi:- Hii ni ngeni eeh? Lakini kweli. Embe ina Vitamini E, ambayo inatengeneza au huamsha hisia za mapenzi.*Huongeza madini ya Chuma:-
Madini ya chuma yaliyopo kwenye embe husaidia kuongeza madini hayo mwilini na kusaidia upungufu wa damu mwilini. Vitamini C iliyopo kwenye embe, husaidi kuupa mwili uwezo wa kufyoza kiurahisi madini hayo ya chuma, kutoka kwenye vyakula vingine.
