Katika makala iliyopita nilizungumzia vyakula vinavyoweza kusababisha mtu kunenepa sana... kama hukuona makala hiyo soma hapa http://masengwa.blogspot.com/2017/02/hivi-ndio-vyakula-10-vinavyonenepesha.html...MAYAI

MBOGA ZA MAJANI

samaki; samaki wana kiasi kidogo sana cha mafuta, wana protein nyingi ambayo itakuacha muda mrefu ukiwa umeshiba na kukufanya usile sana...lakini pia samaki wana kemikali ya omega 3 ambayo ni muhimu sana kwenye mwili kwani huzuia magonjwa ya moyo na kusaidia kazi ya kuchoma mafuta.

maharage; hichi ni chakula kizuri sana cha asili ambachi kimewakuza watu wengi, kina protini ya kutosha pamoja na fibre yaani nyuzi ambazo ni muhimu sana. lakini pia nguvu au calorie yake ni kidogo sana.

maparachichi; wakati matunda mengine yana sukari nyingi, parachichi zina mafuta na nyuzi ambazo ni muhimu sana kwa afya ya moyo na kupunguza uzito. maparachichi pia yana mafuta aina ya oleic oil ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya mizaituni au olive oil na hua yana maji mengi na kumfanya mlaji kutoishiwa maji mwilini.

karanga na korosho; japokua vyakula hivi vina mafuta, mafuta yake ni salama sana hayanenepeshi kama mfuta yatokanayo na wanyama...tafiti zinaonyesha kwamba mafuta haya huweza kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.

matunda; matunda yote unayofahamu yanapunguza uzito isipokua machache yenye sukari nyingi kama ndizi mbivu na zabibu..tafiti zimeonyesha watu wanaokula matunda mengi hua wanakula chakula kidogo sana sababu mafasi kubwa ya tumbo inachukuliwa na matunda ambayo hayaongezi uzito.

nyama ya kuku; hasa kuku wa kienyeji ambao wanakuzwa kiasilia, huwa na protein nyingi sana ambayo inajenga misuli badala ya kuongeza mafuta mwilini, kuku wa kisasa wana kemikali nyingi sana ambazo zinahusiana na magonjwa hatari kama kansa na kadhalika. kumbuka kama unakula kuku kupunguza uzito usile ngozi yake kwani ina mafuta mengi.

mafuta ya maji; mafuta yanayokuja kwa mfumo wa maji kama korie, mafuta ya nazi na alizeti ni mazuri sana kwani yakiingia mwilini hubaki kwenye mfumo ule ule lakini mafuta yanayokuja kwa mfumo wa kuganda kama kimbo, blueband na siagi sio mazuri kwani yakifika tumboni huganda vilevile.

viazi mviringo vya kuchemsha; japokua watu wengi hawataki viazi hivi na kuamua kuvikaanga kila wakati ili wale kama chips lakini ni chakula kizuri sana kama unataka kupunguza uzito..vina sukari kidogo na kiasi kikubwa cha potassium..

maziwa; tofauti na watu walivyokua wanafikiria zamani kuhusu maziwa kwamba yananenepesha sana, utafiti umeonyesha maziwa yanasaidia kupunguza uzito kwani yana kiasi kikubwa cha calcium ambacho husaidia kuchoma mafuta mwilini.

STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183