miti shamba ni nini?
huu ni utaalamu wa matibabu ya binadamu kwa kutumia mimea asilia inayopatikana sehemu mbalimbali, asilimia 25 ya dawa zinazotengenezwa viwandani hutokana na mimea asilia.
nchi zilizoendelea wataalamu wa matibabu haya wanasomea kabisa vyuoni na kupata degree za matibabu haya tofauti na hapa kwetu ambapo mtu yeyote anaweza akaibuka tu na kujiita daktari wa mitishamba, kwa mfano china kusomea udaktari huu wa mitishamba ni miaka mitano na mtu anayesomea lazima awe amaefaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita.
miaka ya hivi karibuni watu wengi hapa nchini tanzania na duniani kwa ujumla wamegeukia dawa hizi na kupenda kuzitumia kuliko zile za hospitali ambazo nyingi hutengenezwa kiwandani.
dawa hizi zimekua zikipingwa sana na madaktari waliosemea elimu ya kisasa yaani madaktari wa kawaida japokua dawa zao nyingi zimetoka kwenye mimea kama nilivyosema hapo mwanzo..mfano kwinini za malaria, digoxin za kutibu moyo na na dawa za aspirini za maumivu ni dawa zinazotokana na magome ya miti..
leo ntaenda kuzungumzia faida na hasara za dawa hizi ili mtumiaji atumie akijua kabisa anapata nini kutoka huko na ntaanza na faida zake kama ifuatavyo...
dawa hizi hazina madhara madogo madogo wakati wa matumizi; mara nyingi dawa hizi za viwandani zikitumika hua na madhara fulani fulani wakati wa matumizi kama kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kadhalika lakini mitishamba watu wengi wameonyesha kuivumilia.
ni mbadala wa dawa za hospitalini; baadhi ya magonjwa ambayo wataalamu hua wanashindwa kuyapatia ufumbuzi wa moja kwa moja kuna baadhi ya mitishamba imeweza kuyatuliza japokua sio kuyatibu kabisa kama kuna dawa mbadala za presha, kisukari, pumu, kifafa na magonjwa mbalimbali yasiyotibika.
zinapatikana kwa wingi sana; dawa hizi ziko sehemu nyingi sana hasa bara la afrika na asia, na kwa mtu anayefahamu anaweza kupanda hata miche kadhaa nyumbani kwake au shambani na kuzitumia pale anapopata tatizo...nakumbuka nilipokua mdogo nilipakwa majani fulani yalikua yameota pembeni ya nyumba nikapona jipu bila hata kulipasua.
bei yake ni ya chini; tofauti na dawa za hospitali ambazo ni gharama sana kuzinunua, dawa za miti shamba ni bei nzuri kwa watu waaminifu lakini hapa kwetu tanzania wametokea watu wajanja wajanja na wanaziuza bei kali sana ambayo sio kawaida.utakuta dozi moja inauzwa laki tano mpaka milioni moja.
Hebu tuone hasara za matumizi ya dawa hizi za mitishamba
1. Hazifai kutumika kwa magonjwa mengi;
2. Hazina dozi inayo eleweka;
3. Huingiliana na dawa za hospitali;
4. Kukosa usimamizi wa dawa hizi;
5. Kuuza vitu ambavyo si vyenyewe;
6. Vifo vya kuepukika;
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
