MWANAMKE ALIYEFUKUA KABURI LA MWANAE ANASWA

Hili ndiyo jeneza likiwa kwenye gari ya polisi kuelekea katika Hospitali ya Ifisi.

Jeshi la polisi wakiwa wamebeba jeneza pamoja na watuhumiwa ambao wameusika katika kufukua Mwili huo 
Mara baada ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba ya Luth.
Wananchi wakishuhudia tukio-(Picha na Ezekiel Kamanga Mbeya) 

Luth Segeleti (52)mkazi wa shigamba Mbalizi Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya baada ya kufukua kaburi la mtoto wake kisha mwili kurudi nao nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya maombi ili afufuke.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema marehemu Baraka Mwafongo (22)alifariki February 15 na mazishi kufanyika Februari 16 mwaka huu, lakini mama Mzazi Luth Segeleti anayeabudu Kanisa la Ufufuo na Uzima alidai mwanawe atafufuka siku ya tatu. 

Kidavashari amesema kuwa Luth alianza zoezi la ufukuaji saa sita usiku na kumaliza zoezi hilo mapema alfajiri kwa kushirikiana na vijana wawili akiwemo mwanawe.

Aidha aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda nao nyumbani kwake kisha kuogesha na kuupaka mafuta tayari kwa maombi.

Hata hivyo baadhi ya majirani walimtilia shaka Luth baada ya kumkuta na jembe akiwa ametoka makaburini na walipomuuliza alikiri kufukua na kudai kuwa mwanawe hajafa hivyo atafufuka baada ya maombi.

Wananchi walitoa taarifa Polisi ambao walifika eneo la tukio na kumhoji Luth ambapo alikiri kufukua kaburi la mtoto wake hivyo Polisi walichukua jeneza tupu na mwili kuupeleka hospitali teule ya Ifisi kwa uchunguzi zaidi. 

Mara baada ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba ya Luth ambapo Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi wakiongoza na mkuu wa Polisi Wilaya hiyo Debora Mrema kufanya kazi ya ziara kuzima moto huo.

Baadhi ya watu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo la uchomaji moto

Mbeya. Wananchi waliojichukulia sheria mikononi wamechoma nyumba ya mama mmoja eneo Mbalizi mkoani hapa, akituhumiwa kufukua maiti ya mwanawe, kuiogesha na kuihifadhi ndani nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amethibitisha kushikiliwa kwa mwanamke huyo.
Amesema tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina limetokea katika Mtaa wa Shigamba, Kata ya Mbalizi.
Inadaiwa baada ya mtoto wake kufariki dunia, mama huyo aliamini angefufuka siku ya tatu, jambo ambalo halikutokea hivyo aliamua kwenda kufukua kaburi na kumtoa.


Tukio zima lilikuwa hivi:
Tukio hilo limetokea mkoa wa Mbeya vijini Mbalizi katika tarafa ya utengule usongwe kitongoji cha Shigamba ambacho kipo barabara ya kwenda Unalike. Marehemu ni kijana mwenye umri wa miaka 22 na alifariki tarehe 16feb17 na kuzikwa tarehe hiyohiyo eneo na makaburini Shigamba barabara ya kwenda umalila. Isuzu wa kuamkia leo ikaonekana kaburi la kijana huyo limefukuliwa na Mama yake mzazi


Inasadikika na Mama yake mzazi akishirikiana na ndugu wa karibu kutokana na imani ya dini yao kwamba mwanae baada ya siku tatu atafufuka.baada ya kufukilwa walibeba

Mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani eneo la shigamba wakauosha na kuuvika suti wakisubiri siku tatu zifike ili aweze kufufuka Kama bwana wetu Yesu Kristu, Mwili wa marehemu umechukuliwa  na polisi pamoja na Mama mzazi kwa uchunguzi zaidi.