TAARIFA zilizotufikia hivi punde kutoka mkoani Kilimanjaro Kaskazini mwa Tanzania, zinaeleza kwamba waandishi wa Habari wawili wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.Waliokamatwa ni Rodrick Mushi wa Tanzania Daima na Gifti Mongi wa Gazeti la Majira na ZBC.
"Gift Mongi alikamatwa jana jioni na kuwekwa Mahabusu katika kituo cha Polisi Majengo huku Rodrick akikamatwa katika ofisi ya RPC akiwa na baadhi ya waandishi wenzake wakifuatilia kisa cha kukamatwa Gift" kimeeleza moja ya chanzo chetu
***** Hii hapa taarifa kutoka Klabu waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro*****
Sakata la kushikiliwa na kuhojiwa waandishi wawili mkoani hapa Gift Mongi na Rodrick Mushi ni kweli ila bado linashughulikiwa na idara ya upelelezi mkoa Kilimanjaro.