Naibu kamishna wa Uhamiaji na Afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara Rose Mhagama amewaambia waandishi wa habari kuwa mpaka sasa amepokea watanzania waliofukuzwa nchini Msumbuji Mia moja na Themanini.
Wakiwa mkoani Mtwara nchini Tanzania raia hao waliofukuzwa nchini Msumbiji wamesema kuwa vitendo vya unyanyasaji vimefanyika dhidi yao vikiwemo vya uporaji ambao wengine wamemueleza mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda kuwa wamefanyiwa vitendo vya ubakaji.
