BREAKING NEWS: BASI LAGONGANA USO KWA USO NA GARI NDOGO SHINYANGA, WAWILI WAUMIA NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPTALI YA RUFAA SHINYANGA

Basi la RUKSA CLASSIC lenye namba za usajiri T636AWC lililokuwa likitokea  Mwanza kwenda Kigoma, limegongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajiri T 210 DJJ katika kijiji cha NHELEGANI mkabala na chuo cha Ushirika Moshi kambi ya Kizumbi manspaa ya Shinyanga mjini muda wa saa nne asubuhi.

Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni uzembe wa dereva wa gari ndogo ambaye muda mwingi alikuwa hatulii barabarani na kujikuta yupo upande usio sahihi na kusababisha ajali.

Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyekufa bali dereva wa gari dogo akiwa na abiria wake mmoja, wameumia na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga ikiwa abiria ameumia zaidi.

Mwandishi mkuu wa MASENGWA BLOG Isaac Luhende alifika eneo la tukio mapema kabisa na ametuletea picha kadhaaa za tukio hilo.

Basi likiwa limevaana uso kwa uso na gari dogo

Basi la RUKSA CLASSIC

Gari dogo likiwa limefunikwa

T636 AWC


Mbele ya basi

Watu wakisaidia kuichomoa gari hiyo

Hivi ndivyo ilivyoharibika gari hii ndogo

Watu wakishuhudia tukio hilo

Nyuma ya gari dogo















PICHA ZOTE KWA HISANI YA MASENGWA BLOG