Kufikia wakati huo, betri ya hedifoni hizo pamoja na kifuniko chake cha plastiki vilikuwa vimeyeyuka na kukwamilia sakafuni.
"Kwa sehemu iliyosalia ya safari, abiria walilazimika kuvumilia harufu kali ya plastiki zilizokuwa zimeyeyuka, vipande vya hedifoni hiyo zilivyokuwa vimeungua na nywele za mwanamke huyo ambazo zilichomeka pia," ATSB walisema kupitia ripoti baadaye.
Ripoti hiyo haikusema hedifoni hizo zilikuwa za muundo gani lakini inaaminika kwamba huenda mlipuko huo ulisababishwa na kasoro kwenye betri za lithium-ion zinazotumiwa katika hedifoni hizo.
Simu za Galaxy Note 7 zilikuwa zinashika moto mwaka 2016
ATSB imechangisha mwongozo kuhusu betri na vifaa vingine vinavyotumia betri.
Kumetokea visa kadha vya vifaa vyenye betri za lithium kulipuka na kushika moto kwenye ndege miaka ya hivi karibuni.
Mwaka uliopita, ndege iliyokuwa inajiandaa kupaa kutoka Sydney iliahirisha safari yake kwa muda baada ya moshi kuonekana ukifuka kutoka kwa mkoba uliokuwa umebebwa na abiria.
Baada ya kukaguliwa, ilibainika kwamba kulikuwa na betri ya lithium iliyokuwa imeshika moto.
Mwaka uliopita pia, kasoro kwenye betri zilitambuliwa kuwa chanzo cha simu nyingi aina ya Samsung Note 7 kulipuka na kushika moto.
Samsung ilisitisha utengenezaji na uuzaji wa simu hizo.


