Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.
Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo pamoja na wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa CCM, Mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wastaafu wa Serikali na kichama walipowasili kwenye ukumbi wa mkutano na kukaribishwa na wajumbe.
Mabalozi na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiwa wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,mjini Dodoma.







