Tangazo la siku 14 kwa TANESCO kuhakikisha wanalipa fidia ya maeneo hayo ambayo ni zaidi ya miaka 3 sasa wameshindwa kuyaendeleza limekuja baada ya wakazi hao kutokuridhishwa na majibu ya maafisa wa TANESCO.
Mwenyekiti wa eneo hilo Bw Elnisha Mshana amesema wamefuata taratibu zote stahiki za kimawasiliano bila muafaka wowote,kwani ni muda sasa wameshindwa kuyaendeleza maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kufanya kilimo cha aina yoyote ile kwani walipigwa marufuku.
Msaidizi mkurugenzi mtendaji uzalishaji kutoka TANESCO licha ya kukiri uwepo wa madai ya zaidi ya shilingi bilioni 22 kama fidia kwa kaya hizo amesema juhudi nyingi zinafanyika ili kuhakikisha ndani ya kipindi kifupi tu fedha hizo zinalipwa na kwa wakati.
Tamthimini ya awali kwa kaya hizo iliyofanywa na maafisa wa wilaya ya Pwani ilionyesha zaidi ya shilingi bilioni 22 zinahitajika ilikulipa fidia kwa wakazi hao, ambapo sasa TANESCO inasema TANESCO wanasema wako katika hatua za mwisho za kuzifanyia uhakiki fedha hizo kabla ya kufanya malipo kwa wakazi hao.
