GARI LAGONGA WATU KADHAA LONDON

Eneo tukio lilipotokea kaskazini mwa London

Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari la mizigo kuvamia kundi la waenda kwa miguu, karibu na msikiti ulioko kaskazini ya mji mkuu wa Uingereza London.

Waziri mkuu Theresa May amekitaja kuwa kisa kibaya akisema kuwa fikra zake ziko kwa wale waliojeruhiwa, wapendwa wao na watoa huduma za dharura eneo hilo.Polisi waimarisha ulinzi

Idara ya kutoa hudum za dharura mjini Lanodn imesema imetuma huduma kadha eneo hilo.

Video iliyowekwea katika mitandao ya kijamii ilionyesha vurugu huku watu wakiwasaidia wale waliojeruhiwa.

Tayari mtu moja amekamatwa kufuatia shambulio hilo lililotokea katika wilaya ya Finsbury Park.Gari lagonga watu kadha London

Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhan.
Gari lagonga watu kadha London

Video zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu walio katika taharuki, kuhu wakijaribu kuwasaidia majeruhi