PICHA: MASTAA MBALIMBALI JINSI WALIVYOHUDHURIA HARUSI YA STAA WA ZAMANI WA BARCELONA

Ijumaa ya June 9 2017 staa wa zamani wa timu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania golikipa Victor Valdes aliamua kuingia katika historia mpya katika maisha yake baada ya kufunga ndoa na Yolanda Cardona.
Harusi ya Victor Valdes na mpenzi wake wa muda mrefu Yolanda Cardona ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali aliwahi kucheza nao soka kama Samuel Eto’o, Keita, Xavi, Eric Abidal, Carles Puyol na golipa namba mbili wake akicheza Barcelona Pinto.
Carls Puyol na mpenzi wake Vanessa Lorenzo

Valdes ambaye kwa sasa anaichezea Middlesbrough ya England alifunga ndoa hiyo na mpenzi wake Yolanda Cardona jijini Barcelona jana Ijumaa ya June 9 2017, kama hujui Yolanda Cardona ni model wa Colombia.

Kushoto ni Abidal na Keita
Kwa mbali mke wa Eto’o na Samuel Eto’o mwenyewe pamoja na Keita
Aliyekuwa golikipa namba 2 wa Barcelona Pinto wakati Valdes akicheza Barcelona.
Puyol na Seydou Keita

Xavi Hernandez na mkewe