SINGIDA UNITED YAMSAJILI MFUNGAJI BORA RWANDA


SINGIDA UNITED YAMSAJILI MFUNGAJI BORA RWANDA


Zile tetesi ambazo zilianza kuenea katika mitandao ya habari za michezo mbalimbali nchini Rwanda kuhusiana na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Rwanda anayeichezea timu ya Polisi FC inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda Danny Usengimana zimethibitishwa 

Singida United ambao walikuwa wamekaa kimya bila kusema chochote kuhusiana na kumfuatilia Danny Usengimana, leo June 17 wamethibitisha kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili, Danny msimu wa Ligi Kuu Rwanda uliyomalizika aliibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 19.