Kuna tunu na upendo wa dhati pale ambapo wamanume ataonesha kujali kwa mwanamke haswa ampendae kwa dhatii ama mke wake, lakin kuna baadhi ya tabia wanaume wanazifanya ambazo zimekuwa zikikera kwa wapenzi wao baadhi ni kama zifuatazo,
1 MUME WA WENGI
Hii ni aina ya wanaume wanaojifanya ni wasamaria wema kwa wanawake wao kias kwamba usamaria wao hautokei kwa wanaume wenzao bali unatokea kwa wanawawke tuu, wanaume wa namna hii wanajali marafiki wa kike wa mke wake tofaut hata na mke wake. mke anaweza kuwa na shida asisaidiwe lakin akatoa pesa kwa mwanamke mwingine aliyemuelezeda shida zake. wanaume wa namna hii unakuta wana marafiki wengi wa kike na zaidi huwa hawaachani na wanawake wao wa zamani, na hata kama wakiaachana utakuta bado anaendelea kumsaidia kwa kila kitu.
2.WANAOJIFANYA WAGUMU
hawa ni aina ya wanaume wanaojifanya hawana mahaba kwa wake zao na wanajifanya wapo biza kila saa na kila wakati na kazi hawa hjua kuwa jukum la ndoa ni kuleta chakula tu ndani na kushughulika na tendo la ndoa kitandani. hana muda wakuzungumza na hajali hata hisia za mke wake, mke akizungumza hata hasikilizwii, anakuwa kidume, anaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mabo ya kuike yaani haoneshi juhud zozote za kumfurahisha mke wake.
3. WANAOPENDA KUTUMIA WAKE ZAO
Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakin wao wala hawajali. wanapowahitaji wanawake waafanyie mambo mazuri basi wao huja na lugha nzuri, maneno mazuri, na hata kuleta vizawadi. Wanajua udhaifu wa wake zao na huwa wanautumia kuwalaghai ili kutimiziwa mahitajiu yao na wakisha timiziwa huwa wanasahau kabixa na hata hawajali tena.
4.WATALII
Hawa ni aina ya wanaume wanaorudi nyumbani kama watalii, yaani ataihudumia familia kwa kila kitu lakini cio kukaa na hiyo familia , wanaume wa aina hii wao kurudi saa nane kwao ni kawaida na huwez ukajua kana mi siku ya off ama yupo kazini, akirudi anamkuta mke na watoto wamelala na kuanza kugonga mlango na hana hata sababu za kuchelewa kwa kias hicho. Hata mwisho wa wiki hupenda kuitumia na marafiki lakin sio kukaa na mke ama familia, hakuna kitu ana cha pamoja ambacho hufanya na mkewe ama watoto wake na kila amara aingiapo ndani huwa ana safari zakutoka.