MTANGAZAJI WA EFM SETH KITENDE 'BIKIRA WA KISUKUMA" AMEFARIKI DUNIA


Mtangazaji wa kituo cha radio EFM cha Jijini Dar es salaam ambaye alikuwa anatangaza kipindi cha Ubaoni Seth Kitende maarufu kwa jina ‘Bikira wa Kisukuma’ amefariki dunia leo jioni Jumapili Julai 9,2017.

Taarifa za awali zinasema Seth amefariki akiwa kwenye Hospitali ya taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Seth Katende alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania akifahamika kwa jina la ‘Bikira wa Kisukuma’ ambapo baadae alianza kufanya kazi ya Radio kwenye kituo cha EFM.

Msiba upo nyumbani kwa baba yake Changanyikeni Dar es salaam.