HARUNA NIYONZIMA AKIRI KIWANGO CHAKE CHA YANGA KUSHUKA AKIWA SIMBA...AELEZA SABABU

Kiungo wa zamanai wa Klabu ya Yanga ambaye kwasasa anacheza katika Klabu ya Simba Haruna Niyonzima amekubali kuwa Kiwango chake cha Simba kinaonekana kuwa cha kawaida sana kulinganisha na alipokuwa Yanga.

Niyonzima amesema SABABU Kubwa inayosababisha kiwango chake kuonekana si kama cha zamani (Akiwa Yanga) kinatokana na Kutokuwa na Maandalizi mazuri kabla ya Msimu (Pre Season)

Niyonzima amesema hayo alipokuwa akiongea kupitia Kipindi cha Spoti Hausi Kinachorushwa na Global Tv.

Kusema Haruna Hajawa Vizuri mimi naweza kusema ni kweli kwasababu wakati najiunga na Simba ofcourse nilikuwa sipo na nilikuwa na baadhi ya Vitu nilikuwa navifanya katika future yangu ya Kesho ambavyo vimenifanya nikachelewa kujiunga na timu lakini timu ilikuwa inajua na Tulikubaliana wakati wananitafuta niliwaambia kuna vitu vitanichelewesha na wakakubali,Lakini kikubwa niko Simba na naamini nitafanya Vizuri.

Haruna alikuwa akichukua kozi ya Ukocha Leseni si wakati ambao Kikosi cha Simba Kilikuwa kimeshaanza Maandalizi ya Msimu, amesema pia Watu wawe wavumilivu na kinachompa matumaini ni kwamba watanzania wengi wanafahamu uwezo wake hivyo wawe na subira mambo yatakaa sawa