HAJI MANARA AWAJIA JUU MASHABIKI WA YANGA

KLABU ya Yanga hivi karibuni ilifanikiwa kupiga hatua na kuingia katika utaratibu mpya wa kuanza kutoa magazine ya klabu itakayokuwa inatolewa mara nne kwa mwaka.
Yanga walitangaza kuwa watakuwa wanatoa magazine inayohusiana na mambo mbalimbali kuhusu klabu yao, historia za wachezaji wao na mambo mbalimbali ya timu hiyo.

Yanga magazine itakuwa inatolewa mara nne kwa mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu, baada ya habari hizo kutoka na magazine hiyo kuanza kusambaa mtaani, mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga walianza kucomment na kumwambia Afisa Habari wa Simba Haji Sandey Manara afanye utaratibu kama huo kwani Yanga ni mfano wa kuigwa.
Baada ya Haji Manara kuona comment hiyo akajibu "Simba ishavuka huko kwenye makaratasi dunia ya sasa ipo kiganjani sisi tunatoa magazine kila mwezi kwenye app ya club"

"Kijarida cha kufungia maandazi? Nenda kwenye app yetu kaone monthly magazine zetu halafu ndio uniletee hicho kijarida chenu"

Post a Comment

0 Comments