WIMBO WA ZILIPENDWA WAMUWEKA MATATANI DIAMOND PLUTNUMZ

Bendi kongwe ya mziki nchini Tanzania ya Msondo Ngoma imeitaka lebo ya WCB iwalipe kiasi cha shillingi milioni 300 kwa kutumia kionjo cha saksifoni ambacho kilipigwa katika waimbo wao mkongwe wa ajali kutumika katika wimbo wa WCB uitwao zilipendwa.

Wimbo huo uliwakutanisha lebo nzima ya WCB na wakawa wameutoa wimbo huo ukiwa na sampo ya kionjo hicho cha wimbo wa msondo ngoma ambao ulitoka kitambo sana uitwao AJALI. Na sasa kupitia wanasheri wa MAXING ADVOCATE, Msondo Ngoma imewaandikia barua WCB ikiwataka wailipe kiasi hicho cha fedha pamoja na kueleza ni kwanini waliamua kufanya hivyo.

Tarehe 25/08/2017 WCB chini ya mwanamziki maarufu nchini Tanzani Diamond Plutnumz, walitoa wimbo wao wa Zilipendwa na wimbo huo uliimbwa kwa kushirikisha wasanii watano ambao ni Diamond Plutnumz, Rayvany, Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darlin

Post a Comment

0 Comments